Mradi wa kuendeleza biashara za wazawa Tanzania

Swahili
Mradi unasaidia wajasiriamali wadogo hasa wanawake kukabiliana na vikwazo na changamoto wanazokutana nazo katika shughuli za uzalishaji kwenye sekta za madini na kilimo. Lengo likiwa ni kuimarisha ubora wa bidhaa na utaratibu mzuri wa huduma zitolewazo kulingana na mahitaji ya soko.
 
Mradi unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza, Iringa, Lindi na Mtwara lengo kubwa likiwa ni kusaidia kuwa na usawa katika ukuaji wa kiuchumi kwa wanawake na wanaume.Mradi unafadhiriwa na Serikali za Canada na Australia.Washirika wengine katika mradi huu ni Taasisi ya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA), SIDO na Taasisi ya Biashara ya wanawake.