Mradi wa kuwezesha bidhaa za wajasiriamali kufikia viwango vya kimataifa

Swahili

SIDO imeingia makubaliano na shirika la ITC kujenga uwezo wa wajasiriamali wadogo kuboresha bidhaa zao kufikia viwango vya kimataifa. Mradi huu unalenga kuboresha mazao makuu matatu ambayo ni Maembe, Viungo na Asali na vilevile kujenga uwezo wa SIDO ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha vifungashio. Mtaalamu wa kufanya upembuzi yakinifu kuhusiana na kuanzisha kituo cha kufunga kuchambua na ‘kugrade’ amekwishapewa kazi tayari. Mpaka sasa mafunzo ya kuweka mfumo wa masoko kwa wajasiriamali 30 yamefanyika. Mradi huu unafadhiriwa na Serikali ya Finland kupitia ITC