Ms.Bhoke Manyori anaisifu SIDO

 

Ms.Bhoke Manyori

Ni mwanamke mjasiriamali kutoka mkoa wa Rukwa ambaye anajishighulisha na ushonaji nguo. Alianza shughuli hii mwaka 2007 akiwa na mashine moja tu katika ofisi yake. Ni mteja wa mikopo katika Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, alianza kukopa mwaka 2009 kwa kiwango cha chini cha Tzsh.400, 000/= kutoka katika mfuko wa NEDF. Mpaka sasa ameweza kufikia kiwango cha juu cha Tzsh.1, 500,000/= akiwa amekopa mara 5. Kutokana na kujiunga na mikopo ya SIDO amefanikiwa kukuza biashara yake kwa kuongeza vitendea kazi vya mashine na kufikia mashine sita na kutoa ajira kwa watu sita, Pia anaweza kusomesha watoto wake kwa kuwalipia ada na kukunua kiwanja ambacho anaendelea na ujenzi wa nyumba. Mjasiriamali huyu anaisifia SIDO na kuwataka wajasiriamali wengine wajiunge na SIDO kwani ni shirika zuri linalo wakopesha wajasiriamali kwa riba nafuu ya asilimia 18

 

 

Swahili
Main Image: