PAMBANA KUTIMIZA NDOTO YAKO

Barke Abubakar ni moja ya wajasiriamali wenye mafanikio mkoani Lindi anajishugulisha na ufugaji wa kuku na mifugo mingine kama ng’ombe na mbuzi. Kabla ya kufika hapo safari yake haikuwa rahisi, alidumu na ndoto ya ufugaji kwa muda mrefu, alianza ufugaji wa kuku mwaka 1997 kupitia mtaji aliopata kwa kubana pesa ya matumizi aliyokuwa akiachiwa na mume wake kwa kujenga banda dogo na kununua vifaranga 100. Hata hivyo mambo hayakwenda kama alivyokuwa amepanga kwa vifaranga 65 kufa kwa magonjwa mbalimbali, Ilimpa wakati mgumu maana yeye mwenyewe hakuwa na elimu yeyote kuhusu ufugaji wa kuku.
Hakukata tamaa aliendelea na ufugaji na kutafuta habari mbalimbali zinazohusu ufugaji bora wa kuku na kufanikiwa kupata elimu mbalimbali za ufugaji bora wa kuku.
Mwaka 2007 alifanikiwa kufikisha kuku 800 wa mayai na nyama na hakapata kikwazo kipya cha kukosa wateja wa mayai na kuku wa nyama. Aliamua kutafta wataalamu mbalimbali ili kupata elimu ya masoko na ndipo alikutana na wataalamu wa SIDO na kufanikiwa kupata ushauri na mafunzo mbalimbali kuhusiana na ujasiriamali na utafutaji wa soko.

Mwaka 2011 SIDO walimuunganisha na mradi wa BDG alifanikiwa kupata mafunzo ya biashara na kufanikiwa kupewa mtaji kutokana na mpango wake wa biashara. Alitumia pesa hiyo kuboresha mabanda ya kuku na kujenga mabanda mapya hivyo kuongenza idadi ya kuku na kufika 2000.
Hivi sasa soko lake kubwa ni mkoa wa Lindi na Mtwara kwa watu binafsi na hoteli .
Kupitia ufugaji wa kuku ameweza kupata mafanikio mbalimbali kama vile kununua kiwanja na kujenga nyumba, kulipia watoto wake karo, kuanzisha ufugaji wa ng,ombe wa maziwa na mbuzi. Ametoa ajira kwa vijana watatu (3). 
Kwa sasa anamalengo ya kuongeza ufugaji zaidi ili kuendana na kasi iliyopo hivi sasa ya ongezeko la watu na makampuni mbalimbali yanayojishugulisha na uwekezaji katika sekita ya gesi mkoani Lindi

Swahili
Main Image: