Programu ya kujenga uwezo wa Vijana Kujiajiri wenyewe

SIDO imeingia mkataba na Tanzania Entrepreneurship Competitiveness Centre (TECC) kutekeleza mradi wa Kijana Jiajiri ukiwa na lengo kuwezesha vijana kuanzisha biashara zinazotoa ajira kwa vijana kati ya miaka 18 mpaka 35. Mradi una sehemu kuu tatu ambazo ni Mafunzo, ushauri na huduma za fedha.

SIDO ikiwa na jukumu la kutoa mafunzo katika maeneo yaliyochaguliwa ambayo ni Lindi, Mtwara and Dar es Salaam.