SHIRIKA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO (SIDO) YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA KUWAANDAA WALIMU WA WAJASIRIAMALI (TOTs) KUANZIA TAREHE 17/07/2023 HADI 04/08/2023
SIDO imeendelea kuwaandaa walimu wa ujasiriamali kwa kuwapatia mafunzo yanayojulikana kama TOTs ( Training of Trainers). Mafunzo haya yana lengo la kuwaandaa washiriki kuweza kutoa mafunzo kwa wajasiriamali katika fani mbalimbali zikiwemo usindikaji wa vyakula, utengenezaji wa sabuni, batiki na uokaji. Mafunzo haya ya ujasiriamali yamekuwa na mwamko mkubwa ambapo washiriki wa rika mbalimbali wameyahudhuria.
Washiriki hawa ni kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Tabora, Pwani, Kagera, Zanzibar na Morogoro. Washiriki hawa wameonyesha utayari wa kuzidi kuwasaidia wananchi walio wengi kuweza kuongeza thamani malighafi zinazozalishwa hapa nchini.
Pamoja na kupatiwa elimu ya usindikaji wa vyakula, utengenezaji wa sabuni na uokaji, SIDO imehakikisha washiriki wanapatiwa elimu kutoka kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo TRA, TBS, BRELA, WMA, GSI TZ na GCLA. Hii itawasaidia kujua taratibu mbalimbali katika zinazotakiwa katika uanzishaji na uendeshaji wa viwanda vidogo nchini. Washiriki hawa pia watapata fursa ya kutembelea viwanda mbalimbali ili kujionea namna uzalishaji unavyakuwa kutoka kwa wajasiriamali wabobezi kwenye fani za usindika wa bidhaa kama vile maziwa, sausage, maji, achari, viungo, utengenezaji batiki, uokaji, n.k.
Hadi mwisho wa mafunzo haya, washiriki watakuwa na elimu juu ya utengenezaji bidhaa mbalimbali za usindikaji, utengenezaji wa sabuni, utengenezaji wa vikoi, utengenezaji wa batiki, elimu juu ya utengenezaji wa lebo, namna ya kutengeneza na kuunda chapa, chaguzi sahihi za vifungashio na maswala yote ya ufungashaji