SIDO YATOA MAFUNZO YA KUONGEZA THAMANI MAZAO YA BAHARINI (UDUVI) KWA WANAWAKE KUTOKA MKURANGA -PWANI

Katika jitihada za SIDO kushiriki Mkakati wa Uchumi wa Bluu, SIDO Dar es Salaam kwa kushirikiana na  Umoja Fisheries Association (UFIA) wametoa mafunzo ya kuandaa unga wa lishe kwa kutumia uduvi ambayo ni aina ya dagaa wenye virutubisho lishe kwa kiwango kikubwa wanaopatikana baharini. Mafunzo hayo yalitolewa kwa washiriki 28 wakiwemo wawakilishi wawili kutoka Wilaya ya Mkuranga – Mkoa wa Pwani.

Lengo kubwa la mafunzo haya  yaliodumu kwa siku tatu kuanzia tarehe 2-4 Septemba 2024 ilikuwa  ni kuwajengea uwezo wanawake wavuvi  wanaojihusisha na ujasiriamali katika mazao ya Bahari ili waweze kupata mbinu mbalimbali za usinindikaji kwa kutumia uduvi, mbinu za kuanzisha na kuendeleza biashara ili kuweza kujimudu kiuchumi, kutumia vizuri rasilimali bahari na kutunza na mazingira pamoja na mbinu za ufungashaji wa bidhaa.

Wahitimu wa mafunzo haya wameahidiwa na mdhamini wako ambae ni Umoja Fisheries zana maalumu za kuchakata na kukausha uduvi ili kuweza kuzalisha bidhaa bora ikiwepo unga wa lishe unaotikana na Uduvi.  Wakati huohuo SIDO imeshiriki katika   kuwapatia  washiriki hao teknolojia za kuchakata na kuandaa ungalishe utokanao na uduvi , pamoja na utumiaji wa viungo mbalimbali vilivyochanganywa na uduvi
Aidha SIDO itaendelea kuwahudumia wahitimu hao kupitia huduma zake za uendelezaji wa teknolojia, mafunzo na ushauri wa kibiashara, kuwaunganisha na masokom mbalimabli ikiwemo kupitia maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, pamoja na huduma za mikopo  ya kuendeleza biashara zao