WAJASILIAMALI WANUFAIKA NA MKOPO WA SANVN

SANVN Viwanda Scheme ni mpango wa uwezeshaji wananchi kuichumi ili kukabiliana na  changamoto mbalimbali  za uanzishaji na uendelezaji viwanda vidogo na vya kati katika maswala mazima ya  upatikanaji wa ujuzi, masoko na mitaji. Walengwa wa mpango huu ni wajasiriamali wadogo na wa kati wenye viwanda wanao jishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuongeza mnyororo wa thamani.

Mpango huu unaratibiwa na taasisi tano ambazo ni SIDO, Benki ya AZANIA,  NSSF, VETA  NA  NEEC  (SANVN).  SANVN Viwanda scheme inatoa mikopo kwa ajili ya uwezeshaji viwanda kwa wajasiriamali wadogo (milioni 8 hadi milioni hamsini 50) na wajasiriamali wa kati (million 50 hadi milioni mia tano 500).  Riba ya mikopo hii ni asilimia 13 na inatolewa na SIDO kupitia ofisi zote za mikoa zilizopo Tanzania bara.
Ili wajasiriamali  wengi waweze kunufaidika na  mfuko huu, kiwango cha riba ni kidogo sana ukilinganisha na watoa huduma nyingine za kifedha. Kupitia maonesho mbalimbali yanayofanywa na SIDO na hasa maonesho ya 4 ya SIDO Kitaifa - Njombe, wajasiriamali wengi walionekana kuvutiwa na mfuko huu kwa kuwa unatoa kiasi kikubwa  cha fedha na riba yake ni ndogo. Pia wajasiriamali hawa waliongezea kuwa,  vigezo na masharti ya mfuko huu ni rahisi kukidhi ili kuweza kukopesheka.  

Mikopo ya SANVN Viwanda Scheme  imegawanyika katika makundi mawili  ambayo ni  Mikopo ya uwekezaji/mashine, mitambo, (investment loan) na hutolewa  kwa ajili ya ununuzi wa mashine/mitambo ili kuanzisha/kuendeleza viwanda vidogo au vya kati.  Aina ya pili  ni  mikopo isiyo ya kiuwekezaji (working capital loan). Hii ni mikopo itolewayo kwa lengo la kuwezesha shughuli za kiutendaji za kila siku mfano ununuzi wa malighafi, vifungashio, matangazo na gharama zingine za uendeshaji Viwanda