WEST KILIMANJARO DAIRY PRODUCT

 

 

WEST KILIMANJARO DAIRY PRODUCT
“BILA SIDO NILIKUWA GIZANI”
West Kilimanjaro ni Kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa JIBINI, iliyoko Mkoani Kilimanjaro wilayani Siha, West Kilimanjaro dairy products inamilikiwa na ndugu Lucas Kaaya.

Historia ya Mradi.
Wazo la mradi lilianza mwaka 1994 baada ya kuwa anafanya kazi kwa raia mmoja wa kigeni kama mfanyakazi wa ndani, kwa kuona mwajili wake akitengeneza kwa ajili ya matumizi binafsi, ndipo alipovutiwa kutaka kijifunza utengenezaji wa JIBINI. Alianza kujifunza taratibu jinsi ya kutengeneza na alopoona anaelekea kufahamu utengenezaji wa JIBINI aliamua kuacha kazi na kuanza kutengeneza bidhaa hiyo katika chumba kimoja kidogo kilichoko kijijini Ngarenairobi  alinza kwa majaribio kwa kununua maziwa lita 20 na kutengeneza jibini aina ya MOZZARELLA na alipoijaribu kwenye soko kwa kuwatembezea wateja majumbani walinunua na kuanza kumpa oda. Namshukuru Mungu kwa kunikuatanisha na SIDO Mwaka 2006 kwani SIDO walianza kunishauri juu ya kuboresha bidhaa yangu na kunipa Mkopo wa kwanza wa shilingi laki tano (500,000/=) ambapo mkopo huo ulinisaidia sana kuongeza uzalishaji wangu pia kuniwezesha kushiriki maonesho yanayoandaliwa na SIDO kila mwaka.  SIDO ilinishauri kutafuta eneo zuri la kuzaliashia ili niweze kuhama kutoka katika chumba ambacho nilikuwa naishi hapo kijijini Ngarenaidobi ambapo niliweza kupata eneo Sanya Juu ambapo ndiko kilipo kiwanda kwa sasa.
SIDO iliendelea kunikopesha fedha na kuniunganisha na taasisi zingine kama TBS, BRELA na kunitambulisha katika Halmashauri ya Wilaya ya SIHA ili niweze kupata leseni ya bishara. Niliweza kupata mafunzo mbalimbali ya Usindikaji wa Bidhaa za maziwa na Uongozi wa Boishara ambayo yalisaidia sana kuongeza ufahamu wangu katika Ujasiriamali.
Mafanikio.
Moja kati ya mafanikio makubwa niliyoyapata baada ya kusaidiwa na SIDO na kuongezeka kwa uzalishaji  wa bidhaa yangu kutoka kununua lita 20 za maziwa kwa siku mpaka lita kati ya 1500 na 2000 kwa siku na kukua kwa soko la bidhaa zangu ambapo imeniwezesha kujenga kiwanda cha kusindika Maziwa  kidogo lakini chenye mashine za kisasa, pia kujenga nyuma ya kuishi na kuongeza ajira kwa Watanzania wenzangu kutoka ajira ya mtu mmoja mpaka watu 12 kwa sasa pia Wafugaji wapatao 558 wa vijiji vinavyozunguka kiwanda wanauza maziwa yao katika kiwanda cha West Kilimanjaro na kujipatia kipato.
Changamoto za Mradi.
Changamoto kubwa katika mradi kwa sasa ni kupatikana chombo kikibwa cha kuhifadhia maziwa ya ujazo wa lita 10,000 kwa siku “Cooler tank” na vifungashio vya kisasa vyenye uwezo wa kuhimili ushindani kutoka nje.
 

 
Mmiliki wa West Kilimanjaro ndugu Lucas Kaaya katika picha tofauti kiwandani kwake, Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.

 

 

Swahili