KOZI YA USINDIKAJI WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA

Swahili
Malengo: 
Kuwawezesha wahusika kupata ujuzi na kuelezea kiundani kanuni mahsusi za usindikaji wa matunda na mbogamboga na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali,kuhakikisha ubora ,gharama na bei pamoja na utengenezaji wa kikaushio kinachotumia umeme wa sola.
Moduli: 
Jina la moduli: 
Usindikaji wa matunda na mbogamboga
Maelezo ya Moduli: 
1.Kanuni za usindikaji wa chakula. 2.Njia kuu za utunzaji wa matunda na mbogamboga. 3.Usafi na usalama wa chakula. 4.Ubora na kiwango cha chakula. 5.Usindikaji/utunzaji wa bidhaa mbalimbali (bidhaa 5). 6.Vifungashio na lebo. 7.Gharama na bei ya bidhaa. 8.Mchoro wa ramani ya sehemu/eneo la usindikaji. 9.Utengenezaji mwepesi wa kikaushio kinachotumia umeme wa sola Mfano:NRI - Kawanda dryer
Mbinu: 
Chemsha bongo, mafunzo ya maelekezo,majadiliano katika vikundi na uwasilishwaji wa mada, nadharia na mafunzo kwa vitendo.
Kundi Husika Linalolengwa: 
Watu/Wajasiriamali wanaotaka kuwekeza kwenye usindikaji wa matunda na mbogamboga
Ada Ya Programu: 
TZs. 500,000 Kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda wa Kozi: 
wiki mbili