
Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO Rukwa latoa suluhisho la ajira kwa wananchi.
Mafunzo hayo yalifanyika kuanzia tarehe 11.05.2020 mpka tarehe 15.05.2020.
Mafunzo haya yalishirikisha wajasiriamali watatu(3) toka katika Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la Mafunzo hayo yalikuwa ni kutoa ujuzi kwa wajasiriamali katika kuanzisha viwanda vidogo, kutoa ajira na kukuza vipato kwa wananchi.
Washiriki hao walifurahia mafunzo hayo juu ya ujuzi walioupata na kuaidi kwenda kuanzisha viwanda ili kutoa ajira kwa wengine na kukuza vipato.Pia Washiriki walilishukuru Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO kwa kutoa mafunzo hayo na kuaidi kuwa mabalozi kwa wengine ili kuwahamasisha nao kushiriki mafunzo kwa ajili ya kujiongezea kipato.