
Mkoa wa DarEs Salaam ni kati ya mikoa 30 katika Tanzania. Makao Makuu ya mkoa huu yapo DarEs Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya sensa ya mwaka 2012, idadi ya watu katika mkoa huu inafikia 4,364,541 kiasi ambacho ni kikubwa kuliko makadirio ya awali ya watu 3,270,255. Katika kipindi cha miaka kumi (2002-2012) utafiti unaonesha kuwa ongezeko la idadi ya watu inafikia wastani wa asilimia 5.6 kwa mwaka, kiasi hicho ni wastani wa watu 3,3133 kwa kila kilomita ya mraba.