Mradi wa kuhamasisha na kuongeza biashara baina ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki- chini ya ufadhiri wa ITC: 2014 hadi 2016

Swahili
Mradi unalenga kuwajengea uwezo wajasiriamali na kusaidia vyombo vya biashara kuongeza thamani katika mazao ya chakula na kutoa huduma zinazohusiana na kukua kwa biashara ndani ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kusafirisha bidhaa nje ya nchi katika masoko ya kimataifa.Mradi unatekelezwa katika nchi za Kenya(pilipili), Tanzania (asali, maembe na viungo) na Zambia(asali).
 
Mradi umelenga kutatua changamoto zinazowazuia wajasiliamali katika kushiriki ipasavyo kwenye muongezeko wa mnyororo wa thamani. Mradi umelenga kuhusisha makundi ya uzalishaji na vyombo vinavyohamasisha biashara. Kwa Tanzania mradi unafanya kazi na SIDO, Shirikisho la Wakulima wa Maembe(AMAGRO), Taasisi ya Asali Tanzania(THC), Taasisi ya Huduma za Misitu Tanzania(TFS) na Shirika la Taifa la kukuza biashara za ndani na nje (TanTrade).