Mradi wa kuwajengea uwezo wanawake na vijana kwenye kuanzisha miradi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo

Swahili
SIDO imeingia makubaliano na shirika la kimataifa la miradi ya maendeleo (UNDP), kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake na vijana katika wilaya nne za mkoa wa Singida ambazo ni  Manyoni, Ikungi, Iramba na Singida vijijini.
 
Mambo yaliyofanywa hadi sasa ni kuwezesha utambuzi wa mahitaji yao ya mafunzo; kuwezesha wajasiriamali kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho ya Kimataifa Dar es salaam na kuhakikisha wajasiriamali wanakuwa na ushindani katika soko kwa kuwawezesha kupata alama na vyeti vya Ubora na Viwango na kutimiza masharti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa.