Programu ya uwezeshaji wa maendeleo ya mlolongo wa thamani ya mazao ya Korosho, Nyama na Ngozi (3ADI – UNIDO)

Mradi una madhumuni ya kuendeleza mazao ya korosho, nyama na ngozi nchini kwa kuwezesha usindikaji wake ili kupata bidhaa mbalimbali zinazoingizwa katika soko. Utekelezaji wa mradi huu umnahusisha Serikali, Taasisi mbalimbali na sekta binafsi kuchangia kuongeza thamani kwenye mazao husika.

Mradi unatekelezwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi kwa kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji na usindikaji kwa kupitia na kutumia Kongano la Korosho la Mtwara. Chini ya Kongano hilo, zimeanzishwa zana za pamoja (Common Shared Facilities) kwa ajili ya kukamilishia usindikaji wa zao hilo. Vikundi vinane(8) vyenye washiriki 160 vinahusishwa.