Katalogi ya Mafunzo

Catalogi ya Mafunzo imesheheni mkusanyiko wa mafunzo mbalimbali na Maelezo ya mafunzo hayo kwa kina, unapohitaji kupata taarifa zaidi kuhusiana na aina Fulani ya mafunzo catalogi hii ya mafunzo inakupatia maelezo ya kina juu ya mafunzo hayo kuanzia ujumbe uliomo ndani ya mafunzo hayo, njia zitakazotumika katika kutoa mafunzo hayo, wateja waliolengwa na mafunzo hayo, gharama ya mafunzo hayo na muda ambao yatafanyika (siku,wiki au mwezi).

Malengo:
Kuweza kuwapatia wahusika uwezo wa kuweza kusimamia na kutumia mikopo kwa usahihi.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Mbinu za Usimamizi wa Mikopo
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Dhumuni na Malengo. 2.Jukumu la mikopo katika maendeleo. 3.Mzunguko wa mikopo. 4.Uanzishwaji wa usimamizi wa mikopo na taarifa. 5.Uhakika na unafuu 6. Upitiaji wa mikopo 7.Understanding Cost and Production. 8.Four basic tools for Enterprise Analysis.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa kubadilishana uzoefu, mazoezi , majadiliano ya magrupu na uwasilishaji wa mtu binafsi.
Kwa wanaoanza biashara, Waliopo kwenye biashara, Biashara ndogo na za kati.
Ada:
TZs. 100,000 kwa muhusika mmoja(ada,chakula na steshonari)
Muda:
Siku 3
Malengo:
Kuwawezesha wazalishaji wa chumvi kupata ujuzi wa kiteknolojia kwenye uzalishaji wa chumvi.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Usindikaji wa Chumvi.
    Maelezo ya Moduli: 
    1. Uchaguzi na uandaaji wa shamba la chumvi. 2. Usindikaji wa chumvi. 3.Ukaushaji na uvunaji wa chumvi. 4.Uongezaji wa madini kwenye chumvi. 5.Ufungashaji na uhifadhi wa chumvi.
Mbinu za kufundishia:
Chemsha bongo,majadiliano ya kwenye kundi na uwasilishaji,nadharia na mafunzo kwa vitendo.
Watu wanaoanza shughuli za usindikaji chumvi.
Ada:
TZs. 100,000 kwa muhusika mmoja(ada,chakula na steshonari)
Muda:
Wiki Mbili
Malengo:
Mwisho wa programu hii wahusika watakuwa na uwezo wa kusimamia biashara zao kwa usahihi na ufasaha.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Kuimarisha Biashara
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Tabia za Mjasiriamali. 2. Kuandaa wazo la Biashara. 3. Kuainisha mazingira ya ndani na nje ya wazo la Biashara. 4. Usimamizi wa Biashara.
  • Jina la moduli: 
    Kupanua Biashara
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Mipango mikakati ya kupanua Biashara. 2.Tathmini ya ukuzaji wa Biashara. 3.Mikakati ya kukuza Biashara. 4.Uandaaji wa Mpango wa Biashara.
Mbinu za kufundishia:
Njia za CEFE kama vile ushirikishwaji wa wanafunzi, mazoezi, majadiliano katika vikundi, Lecture, uwasilishaji wa mtu mmoja mmoja.
Wanaoanza Biashara , waliomo katika Biashara, viwanda vidogo na vya kati.
Ada:
250,000/= kwa muhusika mmoja (Ada,Chakula na Steshonari)
Muda:
Wiki Mbili
Malengo:
Mwisho wa programu hii wahusika watakuwa na uwezo wa kuanzisha,kubaki na kuendeleza biashara zao.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Moduli na.1 :Kujitambua
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Tabia za Mjasiriamali. 2.Kujitambua katika tabia za Ujasiriamali. 3.Kuvumbua mawazo ya Biashara. 4.Kuainisha mazingira ya ndani na nje katika wazo la Biashara. 5.Kuandaa Mpango wa Biashara.
Mbinu za kufundishia:
Njia za CEFE kama vile ushirikishwaji wa wanafunzi, mazoezi katika makundi na uwasilishaji wa mtu mmoja mmoja.
Wanaoanza Biashara, waliopo katika Biashara, Viwanda vidogo na vya kati.
Ada:
250,000/= kwa muhusika mmoja (Ada,Chakula na Steshonari)
Muda:
Wiki Mbili

Pages