Katalogi ya Mafunzo

Catalogi ya Mafunzo imesheheni mkusanyiko wa mafunzo mbalimbali na Maelezo ya mafunzo hayo kwa kina, unapohitaji kupata taarifa zaidi kuhusiana na aina Fulani ya mafunzo catalogi hii ya mafunzo inakupatia maelezo ya kina juu ya mafunzo hayo kuanzia ujumbe uliomo ndani ya mafunzo hayo, njia zitakazotumika katika kutoa mafunzo hayo, wateja waliolengwa na mafunzo hayo, gharama ya mafunzo hayo na muda ambao yatafanyika (siku,wiki au mwezi).

Malengo:
Nia ya usambazaji wa elimu ya kilimo cha Uyoga ni: - 1. Kupata chakula bora kwa mwaka mzima bila kusubiri msimu wa mvua. 2. Ajira kwa akina Mama na Vijana kwani kinahitaji mtaji mdogo na mazao hupatikana katika muda mfupi. 3.Kujua matumizi rudia ya masalia ya uzalishaji. 4. Kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutumia takataka. 5. Kupata uyoga wenye virutubisho muhimu. 6. Kupunguza matukio ya vifo vitokanavyo na kula uyoga wenye sumu.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Kilimo cha Uyoga
    Maelezo ya Moduli: 
    Moduli ya Kilimo cha Uyoga inazo sehemu kuu tano: - 1. Kuandaa banda la kuoteshea Uyoga. 2. Matayarisho ya Vimeng'enywa, ikiwa ni pamoja na kuvichemsha. 3. Kuweka vvimeng'enywa kwenye mifuko ya plastiki. 4. Kupanda mbegu ya Uyoga kwenye mifuko ya plastiki. 5. Kuhifadhi mifuko iliyopandwa mbegu kwenye chumba cha giza kwa muda wa wiki 2 - 4, kisha itoe chumba cha giza na ining'inize kwenye shelfu ya miti.
Mbinu za kufundishia:
Njia ya mafunzo ni ya ushirikishwaji pamoja na kujifunza kwa vitendo.
Wakulima wapya wa kilimo cha Uyoga.
Ada:
Shilingi za Kitanzania 150,000/= kwa kila mshiriki. ( Hii ni ada pamoja na steshonari)
Muda:
Wiki mbili.

Ifuatayo ni orodha ya vitu vinavyohitajika kama unataka kuingia kwenye kilimo cha Uyoga: -

1. Vimeng'enywa.

2. Panga.

3. Nailoni la kutandika mezani.

4. Meza kubwa.

5. Mbegu ya Uyoga.

6. Banda la kuoteshea Uyoga.

7. Mifuko ya plastiki.

8. Pipa/Sufuria la kuchemshia vimeng'enywa.

9. Kamba ya kufungia mifuko.

10.Kichanja cha kuwekea vimeng'enywa baada ya kuchemshwa. Hiki hujengwa kwa kutumia fito au mianzi.

 

Jinsi ya kulima kilimo hiki lazima upate mafunzo ya Kilimo cha Uyoga.

Malengo:
Wahusika waliolengwa watakuwa na uwezo wa kutengeneza mishumaa na kuanzisha biashara zao.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Utengenezaji wa Mishumaa
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Maana ya Mishumaa. 2.Aina ya nta ya kutengenezea mishumaa. 3. Faida na hasara za nta husika iliyotajwa hapo juu. 4. Vifaa maalumu vinavyohitajika na kutumika katika utengenezaji wa mishumaa. 5. Namna mishumaa inavyotengenezwa (Mafunzo ya nadharia na vitendo). 6. Hatua za ufungashaji wa mishumaa.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa uzoefu,Nadharia, vitendo na michezo.
Wanaotaka kuanza kutengeneza mishumaa.
Ada:
TZs150,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Kuwawezesha wahusika wanaojihusisha na mbao ikiwemo mafundi seremala/waashi, wauzaji mbao za jumla na .............kupata mbinu za kuweza kukausha mbao kuendana na matumizi yake.Kuhamasisha viwanda vidogo na vya kati kutumia mbao za msimu ili kuimarisha ubora wa bidhaa na kushikilia soko.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Uchakataji wa Mbao
    Maelezo ya Moduli: 
    1. Aina ya unyevu 2. Nini kinatokea mbao inapokaushwa. 3. Kwanini mbao inatakiwa kukaushwa kabla ya matumizi? 4. Kiwango cha unyevu 5. Kiwango cha unyevu na matumizi ya mbao. 6. Njia za ukaushaji. 7. .......... wakati wa ukaushaji. 8. Ukaushaji wa njia ya hewa. 9. Ukaushaji wa kutumia paa la nyumba. 10.Udhibiti wa uishaji wa mbao. 11.Namna ya uhifadhi wa mbao. 12.Gharama ya ukaushaji wa njia ya hewa.
Mbinu za kufundishia:
Mafunzo yanatolewa kwa mtaala wa Forest Industries Training Institute(FITI) .Lakini pia Mafunzo yanatolewa kulingana na mahitaji.Mafunzo yanakuwa kwa njia ya ushirikishwaji ,majadiliano kwa makundi,mafunzo kwa njia ya vitendo,mazoezi na kubadilishana uzoefu.
Wawakilishi kutoka viwanda vidogo na vya kati vinavyojihusisha na masuala ya uashi,biashara ya mbao na wajenzi.
Ada:
TZs. 100,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Wateja waliolengwa watakuwa na uwezo wa kutumia vifaa vya TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) kwa lengo la kukuza biashara na ushindani wa kibiashara.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Maana ya TEHAMA(Teknolojia ya Habari na Mawasiliano)
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Vifaa vya TEHAMA na matumizi yake. 2.TEHAMA na biashara. 3.Utafutaji wa taarifa. 4. Huduma za nufuvi. 5.Utunzaji wa kumbukumbu na upitiaji.
Mbinu za kufundishia:
Mfunzo kwa njia ya vitendo
Wanaotaka kuanza biashara,Waliokwisha anza biashara, waliopo kwa muda mrefu na viwanda vidogo na vya kati.
Ada:
TZs. 100,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
Siku tatu
Malengo:
Kuwezesha makundi ya wasindikaji wadogo na wa kati kuongeza kipato mashambani kwa kuwezesha na kuhamasisha utumiaji wa teknolojia sahihi kwenye usindikaji.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Usindikaji wa Korosho
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Uendeshaji na utunzaji wa mashine. 2.Hatua za ubanguaji korosho. 3.Hatua za ukaushaji/ukaangaji wa korosho. 4.Ufungashaji na uhifadhi wa bidhaa za korosho.
Mbinu za kufundishia:
Mafunzo kwa njia ya vitendo.
Watu na makundi yaliyo na nia ya kujihusisha na usindikaji wa zao la Korosho.
Ada:
TZs150,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Kuwawezesha wahusika kupata ujuzi na kuelezea kiundani kanuni mahsusi za usindikaji wa matunda na mbogamboga na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali,kuhakikisha ubora ,gharama na bei pamoja na utengenezaji wa kikaushio kinachotumia umeme wa sola.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Usindikaji wa matunda na mbogamboga
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Kanuni za usindikaji wa chakula. 2.Njia kuu za utunzaji wa matunda na mbogamboga. 3.Usafi na usalama wa chakula. 4.Ubora na kiwango cha chakula. 5.Usindikaji/utunzaji wa bidhaa mbalimbali (bidhaa 5). 6.Vifungashio na lebo. 7.Gharama na bei ya bidhaa. 8.Mchoro wa ramani ya sehemu/eneo la usindikaji. 9.Utengenezaji mwepesi wa kikaushio kinachotumia umeme wa sola Mfano:NRI - Kawanda dryer
Mbinu za kufundishia:
Chemsha bongo, mafunzo ya maelekezo,majadiliano katika vikundi na uwasilishwaji wa mada, nadharia na mafunzo kwa vitendo.
Watu/Wajasiriamali wanaotaka kuwekeza kwenye usindikaji wa matunda na mbogamboga
Ada:
TZs. 500,000 Kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki mbili
Malengo:
Kuwawezesha wahusika kuelewa na kuelezea kwa kina njia za ufugaji nyuki,uvunaji , usindikaji wa asali na masega ya nyuki. Lakini pia Kuhakikisha ubora wa bidhaa na kuelewa vitu gani vinahitajika katika kupata soko.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Usindikaji wa asali na masega ya nyuki
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Kanuni za ufugaji nyuki. 2.Uvunaji wa asali na usindikaji. 3.Uhakika wa ubora wa asali na masega ya nyuki. 4.HACCP katika sekta ya asali. 5.Bar codes
Mbinu za kufundishia:
Viwanda vidogo vinavyohusika na kilimo na usindikaji ikiwemo wasindikaji na wauza vyakula.
Ada:
TZs 200,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Kuwawezesha wasindikaji kujua bidhaa zinazoweza kusindikwa kutokana na fenesi, kujifunza njia za usindikaji wa bidhaa hizo na jinsi ya kuzifungasha. Kujua faida za kulitumia tunda la fenesi.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Bidhaa zinazoweza kusindikwa kutokana na tunda la fenesi
    Maelezo ya Moduli: 
    1. Usafi na Usalama wa bidhaa za fenesi. 2. Udhibiti wa ubora wa bidhaa za fenesi. 3. Vifaa vitakiwavyo na visivyotakiwa katika usindikaji wa bidhaa za fenesi. 4. Mafunzo ya nadharia na vitendo ya usindikaji wa bidhaa za fenesi. 5. Ufungashaji wa bidhaa za fenesi. 6. Gharama na upangaji wa bei.
Mbinu za kufundishia:
Njia ya mafunzo ni ya ushirikishwaji na kujifunza kwa vitendo.
Wasindikaji wapya na waliopo kwenye sekta ya Usindikaji kwa muda mrefu.
Ada:
TZS. 100,000/=
Muda:
Wiki mbili

Fenesi ni tunda kubwa linalopatikana Tanzania. Katika Tanzania linalimwa sana katika ukanda wa pwani. Fenesi linaweza kusindikwa bidhaa zaidi ya saba, na baadhi yao ni kama zifuatazo: -

1. Achali ya fenesi.

2. Jamu ya fenesi.

3. Juisi ya fenesi.

4. Wine ya fenesi.

5. Sirapu ya fenesi

6. Chips za fenesi.

7. Chokoleti za fenesi.

Malengo:
Wahusika watapata ujuzi wa umuhimu wa kudhibiti ubora na ufungashaji mzuri wa bidhaa zao za vyakula.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Ubora wa chakula, Usalama na Ufungashaji.
    Maelezo ya Moduli: 
    1.Maelezo ya mwanzo ya dhana nzima ya ubora wa chakula 2. 3.Usalama na usafi wa vyakula 4.Watu na vifaa (eneo la biashara, jengo na vifaa) 5. Kuelewa dhana ya kilimo bora. 6. Hatua za udhibiti wa majanga. 7. Ufuatiliaji. 8.Vifungashio na Lebo.
Mbinu za kufundishia:
Chemshabongo, Majadiliano ya makundi na uwasilishaji, nadharia na mafunzo ya vitendo.
Ada:
TZs150,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Kuwawezesha wahusika kujifunza na kuanzisha usindikaji wa vyakula katika aina fulani ya bidhaa za vyakula.
Moduli:
  • Jina la moduli: 
    Bidhaa za vyakula maalumu vilivyochaguliwa.
    Maelezo ya Moduli: 
    1. Usafi wa Chakula. 2. Kanuni za ubora na uhakika/Udhibiti wa ubora wa chakula. 3. Mafunzo ya vitendo katika utengenezaji wa chakula. 4. Uandaaji wa mpango wa biashara. -Tabia za Ujasiriamali. -Gharama na upangaji wa bei.
Mbinu za kufundishia:
Njia ya mafunzo ya ushirikishaji/kujifunza kwa vitendo.
Wasindikaji wapya na waliopo kwenye sekta kwa muda mrefu.
Ada:
TZs 250,000 kwa muhusika mmoja(ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja

Pages